Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mshikamano ndio suluhisho zama za sasa za taabu

Mshikamano ndio suluhisho zama za sasa za taabu

Pakua

Katika ulimwengu wa sasa unaoshuhudia migawanyiko, hofu ya vita vya nyuklia na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, Umoja wa Mataifa umeusihi ushirikiano zaidi na umoja miongoni mwa wanachama wa Muungano wa Ulaya, EU.

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito hu oleo huko Brussels, Ubelgiji wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano wake na rais wa EU Jean-Claude Juncker.

 

Guterres amesema vita baridi vimerejea, ingawa ni katika mfumo mwingine, huku uendelezaji wa silaha za nyuklia na kemikali ukishika kasi.

 

Mapinduzi ya nne ya viwanda nayo yanashamiri, yakichagizwa na utandawazi ingawa bado hayajaweza kuwa na manufaa kwa kila mkazi wa dunia.

 

Ni kwa kuzingatia  mazingira hayo Katibu Mkuu amesihi nchi wanachama wa EU waungane zaidi na zaidi na wawe na ufanisi katika mipango yao na kuzungumza kwa sauti moja kwa kuwa hivi sasa umoja ndio msingi wa ushirikiano wa kimataifa.

 

Amezungumzia pia mkataba wa Iran kuhusu nyuklia,  akisema Umoja wa Mataifa unaunga mkono hatua za EU za kunusuru mkataba huo baada ya Marekani kujitoa hivi karibuni.

 

Kuhusu  uhusiano kati ya EU na UN, Bwana Guterres amesema kuwa ni wa mfano wa aina yake katika nyanja zote ikiwemo kifedha, kisiasa na kijamii, hali ambayo inawezesha utekelezaji wa shughuli za Umoja wa Mataifa duniani.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Sauti
1'23"
Photo Credit
Madhara ya mabadiliko ya tabianchi, hasa ukame wa muda mrefu katika Afrika inasababisha kuongezeka kwa njaa ya kimataifa. Picha: UM