Vijana tutumie fursa zilizopo kujikwamua na umasikini: Majd
Tatizo la ajira katika nchi zinazokabiliwa na machafuko ya kivita ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya vijana, kwa sababu wahalifu, waasi na watu wenye itikadi kali hutumia mwanya huo na kuwarubuni vijana hao kujiingiza katika ugaidi na uwaasi.
Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake kama ILO na wadau, wamekuwa bega kwa bega na serikali nyingi duniani kutafuta mbinu za kuwawezesha vijana kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira kupitia ufadhili wa miradi ya vijana, mafunzo ya ujasiriamali ili kuwawezesha vijana kufikia lengo nambari 8 la ajenda ya maendeleo endelevu linalozungumzia ajira bora na ukuaji wa uchumi.
Kwa muktadha huo, mwandishi wetu leo anatupeleka katika mji wa Gaza, huko Palestina ambako msichana mmoja amekuwa chachu na mfano wa kuigwa na jamii yake baada ya kutumia ubunifu wake na kuanzisha miradi ambayo imewapa wananchi wa Gaza matumaini mapya katika masuala ya ujenzi na nishati mbadala. Nini kilichojiri huko?
Ungana na Patrick Newman katika makala hii, upate undani zaidi.