Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili dhidi ya wanawake ni adui ya SDGs

Ukatili dhidi ya wanawake ni adui ya SDGs

Pakua

Wanawake na wasichana, popote pale wanahitaji kuwa na haki na fursa sawa na pia wawe huru kuishi katika mazingira yasiokuwa na ukatili wala ubaguzi. Usawa wa jinsia na uwezeshaji ni lengo namba tano la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs na ni muhimu katika kufikia maendeleo hayo kama yalivyoainishwa na Umoja wa Mataifa. Hata hivyo ukatili majumbani ni moja ya changamoto zinazokwamisha kufikia usawa huo wa jinsia. Je nchini Uganda hali ikoje mwandishi wetu John Kibego anatupeleka moja kwa moja hadi wilaya ya Hoima nchini humo. Ungana naye.

Audio Credit
Grace Kaneiya/John Kibego
Audio Duration
3'32"
Photo Credit
Wanawake nchini Uganda.(Picha:UNFPA)