Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waliopoteza maisha kutokana na mafurikio Kenya wafika 132: OCHA

Waliopoteza maisha kutokana na mafurikio Kenya wafika 132: OCHA

 Waliopoteza maisha  kutokana na mafurikio Kenya  wafika 132: OCHA 

Idadi ya waliokufa kutokana na athari za mafuriko nchini Kenya  imepanda na maelfu wameachwa bila makazi wakihitaji msaada.  Flora Nducha anafafanua zaidi

Ofisi ya shirika la Umoja wa Mataifa inayoratibu masuala ya kibinadamu namisaada ya dharura OCHA linasema kuwa hadi sasa idadi ya waliofarikiimefikia watu132 huku   zaidi ya 311,000 wameachwa bila makazi. Jens Laerke msemaji wa OCHA, amewaelezea  waandishi habari mjini GenevaUswis  kuhusu hali ilivyo sasa

(SAUTI YA LAERKE)

  “Nchi Kenya mvua zinatarajiwa kuendelea kunyesha na kwa mujibu wa idara ya utabiri wa hali ya hewa  hadi mwisho wa mwezi huu na kwa hivyo mafuriko mengine  yanawezekana kutokea.”

 Ameongeza kuwa  kazi ya kujiandaa kwa hali ijayo pamoja na kuwashughulikia walioathirika na mafuriko, na kupata manusura inaendelea,  ambapo tayari watu 132 wamepoteza maisha wakiweko 30 waliofariki baada ya bwawa moja  sehemu za Nakuru kufurika,. Shughuli hizo za ukozo na misaada zinafanywa na serikali ya Kenya kwa ushirikiano na wadau kikiwemo chama cha msalaba mwekundu na shirika la kuhudumia watoto la umoja wa Mataifa UNICEF.

 Na kuhusu nchi jirani za Somalia na Ethiopia amesema

 (SAUTI YA LAERKE)

 “ Nchini Somalia mvua  kali zinaendelea  katika mabonde ya mito ya Juba na Shebelle na zinasababisha mito kufurika na kuathiri watu 718,000 wa maeneo hayo huku watu 220,000 wameachwa bila makazi.”

Pakua

Ofisi ya shirika la Umoja wa Mataifa inayoratibu masuala ya kibinadamu namisaada ya dharura OCHA linasema kuwa hadi sasa idadi ya waliofarikiimefikia watu132 huku   zaidi ya 311,000 wameachwa bila makazi. Jens Laerke msemaji wa OCHA, amewaelezea  waandishi habari mjini GenevaUswis  kuhusu hali ilivyo sasa

(SAUTI YA LAERKE)

  “Nchi Kenya mvua zinatarajiwa kuendelea kunyesha na kwa mujibu wa idara ya utabiri wa hali ya hewa  hadi mwisho wa mwezi huu na kwa hivyo mafuriko mengine  yanawezekana kutokea.”

 Ameongeza kuwa  kazi ya kujiandaa kwa hali ijayo pamoja na kuwashughulikia walioathirika na mafuriko, na kupata manusura inaendelea,  ambapo tayari watu 132 wamepoteza maisha wakiweko 30 waliofariki baada ya bwawa moja  sehemu za Nakuru kufurika. Shughuli hizo za ukozo na misaada zinafanywa na serikali ya Kenya kwa ushirikiano na wadau kikiwemo chama cha msalaba mwekundu na shirika la kuhudumia watoto la umoja wa Mataifa UNICEF.

 Na kuhusu nchi jirani za Somalia na Ethiopia amesema

 (SAUTI YA LAERKE2)

 “ Nchini Somalia mvua  kali zinaendelea  katika mabonde ya mito ya Juba na Shebelle na zinasababisha mito kufurika na kuathiri watu 718,000 wa maeneo hayo huku watu 220,000 wameachwa bila makazi.

Audio Credit
Patrick Newman
Audio Duration
1'42"
Photo Credit
Picha ya Umoja wa Mataifa