Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaala wa ujasiriamali wawezesha wanafunzi Msumbiji kujikimu

Mtaala wa ujasiriamali wawezesha wanafunzi Msumbiji kujikimu

Pakua

Barani Afrika idadi ya vijana kama ilivyo katika mabara mengine inaongezeka kila uchao. Kasi ya ongezeko hilo haiendi sambamba na mabadiliko ya stadi shuleni ili waweze kupata ujuzi wa kuwawezesha kukabiliana na maisha yao. Ni kwa kuzingatia hilo, Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la maendeleo ya viwanda, UNIDO limeanzisha mradi wa kujumuisha mtaala wa ujasiriamali katika shule za msingi na sekondari barani Afrika.

Miongoni mwa nchi zilizoanza kunufaika na mradi huo ni Msumbiji ambako katika makala hii Siraj Kalyango anaangazia kwa kina kilichofanyika na mapokeo ya wanafunzi katika masomo hayo.

Audio Credit
Siraj Kalyango
Audio Duration
3'30"
Photo Credit
Picha: UNFPA/Omar Gharzeddine