Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pengo la ufadhili ladidimiza huduma kwa wakimbizi wa DRC: UNHCR

Pengo la ufadhili ladidimiza huduma kwa wakimbizi wa DRC: UNHCR

Pakua

Kufuatia mmiminiko wa wanaokimbia mizozo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, mashirika ya kibinadamu Uganda yanakumbana na changamoto lukuki kuwahudumai kwani wanaingia ncchini humo kunyume Zaidi na matarajio kinachopanua pengo la ufadhili. 

Msemaji wa Shirika la Umoja wa Maifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR), Uganda, Duniya Aslam Khan ameniambia kuwa pengo la ufahdili limeathiri vibaya juhudi za kushughulikia wakimbizi hao hasa katika sekta za afya na elimu.

Amesema, kwamba kwa sasa wamepokea  aslimia tatu tu ya ombi la ufadhili la dola milioni 504 lililozinguliwa pamoja na wadao wao 30 wa kibinadamu mnamo Machi kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya wakimbizi hao katika mwaka huu 2018.

Fedha hizo zilikuwa zisaidie wakimbizi 60,000 waliotarajiwa kutoka DRC, mnamo 2018, lakini sasa  ikiwa ni miezi mitano pekee, wakimbizi takribani 80,000 tayari wamesajiliwa.

Duniya ameongeza kuwa wanahofia pengo hilo la ufadhili kusababisha madhara makubwa miongoni mwa wakimbizi na jamii zinazowahifadhi.

Amesisitiz akwamba kuna kuna haja leo na sio kehso wahisani kuitikia Zaidi wathirika wa mzozo wa DRC ambao ameutaja kuwa ni wenye changamoto kubwa Zaidi na uliosahaulika.

Audio Credit
John Kibego
Audio Duration
1'11"
Photo Credit
UNHCR/Michele Sibiloni