Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kanuni za mtandao Tanzania zasitishwa kwa muda

Kanuni za mtandao Tanzania zasitishwa kwa muda

Pakua

Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mtwara imezuia kwa muda matumizi ya kanuni mpya za maudhui ya habar iza mtandaoni nchini humo. Kanuni hizo zilikuwa zianze kutumia kesho tarehe 5 Mei 2018, na zinatokana na Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya mwaka 2018.

Kupitia kanuni hizo wamiliki wa blogu, radio na televisheni za mtandaoni wanapaswa kujisajili ili waweze kuendelea kutoa huduma hizo.

Hata hivyo taasisi sita ziliwasilisha malalamiko yao mbele ya mahakama, na leo hii Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Mtwara imeamua kusitisha kwa muda matumizi ya kanuni hizo hadi itakapopitia shauri la msingi la taasisi hizo. Assumpta Massoi wa idhaa ya Umoja wa Mataifa amezungumza na Deodatus Balile, Kaimu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini Tanzania, TEF na kuanza kwa kumuuliza wamepokea vipi uamuzi huo wa mahakama.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
6'8"
Photo Credit
Mitandao ya kijamii imeibuka na faida na changamoto zake hasa iwapo mtumiaji anakuwa hatambui sheria za matumizi. (Picha: World Bank/Arne Hoel)