Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nyumba na mashamba vimetwama kwenye maji, magari ya usafiri yamekwama: Mafuriko Somalia

Nyumba na mashamba vimetwama kwenye maji, magari ya usafiri yamekwama: Mafuriko Somalia

Pakua

Rais wa Somalia Mohammed Abdullahi Mohammed Farmajoo amezuru maeneo yaliyokumbwa na mafuriko nchini humo hususuan maeneo ya kati ya nchi na kusihi jamii ya kimataifa isaidie wasomali 650,000 walioathiriwa na mafuriko hayo nchini kote.

Nats..

Rais Farmajoo na  ujumbe wake wakiwemo maafisa wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika walitumia usafiri wa ndege kukagua na kufika jimbo la kati la Hirshabelle ili kujionea hali halisi. Katika jimbo hili pekee waathirika wa mafuriko ni watu 150,000.

Nyumba na mashamba vimetwama kwenye maji, magari ya usafiri yamekwama kwa kuwa mito imefurika na wananchi hawajui la kufanya.

Akiwa kwenye mji wa Belet Weyne Rais Farmajoo na  ujumbe wake walishuhudia kiwango kikubwa cha maji kilichotwama, na kisha akafunguka.

(Sauti ya Rais Mohamed Abdullahi Mohamed Farmaajo)

 “Tumeunda kamati ya kimataifa ya majanga ambayo serikali inaongoza hatua za kushughulikia mahitaji ya wananchi ambao wameathirika na mafuriko. Tutatumia rasilimali zote zilizopo ili kuwasaidia.”

Ujumbe huu pia uliwatembelea pia wakimbizi wa ndani kwenye kambi ya Eel Jaale ambapo baada ya mazungumzo na raia hao  Naibu Mkurugenzi wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya misaada ya dharua, Yngvil alifunguka.

(Sauti ya Yngvil Foss)

 “Tunaomba msaada zaidi. Tunachukua hatua kwa kadri ya uwezo wetu. Lakini tunaomba fedha zaidi kwa ajili ya malazi, chakula na maji.”

Kwa ujumla mafuriko yameathiri zaidi ya watu 650 na mvua zinazoendelea kunyesha zinatarajiwa kuleta madhara zaidi.

Audio Credit
John Kibego
Audio Duration
1'28"
Photo Credit
UN Photo/Tobin Jones)