Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa elimu watumbukiza wengi kwenye ajira zisizo rasmi- Ripoti

Ukosefu wa elimu watumbukiza wengi kwenye ajira zisizo rasmi- Ripoti

Pakua

Watu bilioni 2 kote ulimwenguni wanafanya kazi katika sekta isiyo rasmi na idadi kubwa ni katika nchi zinazoendelea na zile zinazoibuka kiuchumi.

 

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika la kazi duniani, ILO iliyochapishwa hii leo ikijikita katika takwimu za wanawake na wanaume walio kwenye sekta hiyo.

 

Ripoti inasema idadi hiyo ni zaidi ya asilimia 61 ya watu wote walioajiriwa duniani ikitanabaisha kuwa kiwango kidogo cha elimu ni kichocheo cha watu kuingia kwenye sekta hiyo.

 

Mathalani barani Afrika asilimia 85.6 ya ajira ni katika sekta isiyo rasmi, wanaume wakiwa ni wengi zaidi lakini wanawake ni wengi zaidi kwenye sekta isiyo rasmi iliyo na mazingira duni na magumu zaidi.

 

Mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo Vicky Leung amesema wafanyakazi katika sekta hiyo hawana hifadhi ya jamii, wanafanya kazi katika mazingira duni na haki zao zinabinywa.

 

Kwa mantiki hiyo ametaka hatua zichukuliwe kurasimisha kazi hizo na kubuni mbinu ambazo kwazo zitaendana na mazingira ya kazi na hatimaye kuwa na ajira endelevu zinazojali haki za wafanyakazi.

 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
1'6"
Photo Credit
FAO/Olivier Asselin