Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN na wadau waleta matumaini kwa watoto wakimbizi Rwanda

UN na wadau waleta matumaini kwa watoto wakimbizi Rwanda

Pakua

Watoto wakimbizi nchini Rwanda sasa wanaona nuru katika maisha yao kutokana na ushirikiano kati ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na mfuko wa H&M. 

Ubia huo unawezesha watoto wakimbizi nchini Rwanda kupata elimu kwa kuwa wanaishi katika makazi salama na zaidi ya yote wanapatiwa vifaa vya shule na kuwa na uhakika wa maisha yao ya baadaye.

Miongoni mwa wanufaika wa ushirika huo ni mwanafunzi Godfried kutoka Burundi ambaye sasa anaishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Mahama nchini Rwanda.

Godfried anasema tangu akiwa mtoto mdogo aliwa na ndoto ya kuwa mwandishi wa habari, lakini machafuko nchini Burundi yalififisha ndoto hiyo.

Alilazimika kukimbilia Rwanda ambako sasa angalau nuru inamuangazia.

Nats..

Sasa  yuko salama kambini na ndoto ya Godfried ya kuwa mwandishi wa habari inaonekana kutimia kwa kuwa..

(Sauti ya Godfried)

“Sasa niko salama na ninahudhuria darasani.  Nina furaha kwamba wanatupatia vifaa vya shule .”

UNHCR inasema duniani kote ni asilimia 61 tu ya watoto wakimbizi ndio wana fursa ya kuendelea na masomo ukimbizini.

 

Audio Credit
Selina Jerobon
Audio Duration
1'22"
Photo Credit
UNHCr/Anthony Karumba