Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shambulio la kigaidi Afghanistan laua 14 na kujeruhi Zaidi ya 30: UNAMA

Shambulio la kigaidi Afghanistan laua 14 na kujeruhi Zaidi ya 30: UNAMA

Pakua

Watu takribani 14 wameuawa hii leo na wengine wapatao 0 kujeruhiwa katika mashambulio mawili ya kujitoa muhanga mjini Kabul Afghanistan.

Kwa mujibu wa tarifa iliyotolewa na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA, mashambulio hayo yametokea katika makazi yaliyofurika watu kwenye viunga vya mji wa Kabul yakipishana dakika 30.

Taarifa zinasema baada ya shambulio la kwanza , waandishi wa habari waliwasili kuweza kuripoti na ndipo shambulio la pili likatokea likiwalenga waandishi hao na wafanyakazi wa huduma ya dharura waliofika  kutoa msaada kwa waathirika wa shambulio la kwanza.

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan ambaye pia ni mkuu wa UNAMA Tadamichi Yamamoto amesema mashambulizi haya yanasababisha madhila makubwa yasiyoelezeka kwa familia za Afghanistan.

Ameongeza kuwa amesikitishwa na ana laani vikali mashambulizi hayo ambayo yanaonekana kuwa ni ya makusudi dhidi ya waandishi wa habari ikiwa ni siku chache tu kabla ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani, hivyo  amesema ni mashambulizi ya moja kwa moja dhidi ya uhuru wa kujieleza.

Audio Credit
John Kibego
Audio Duration
1'
Photo Credit
Picha ya UN /Eskinder Debebe