Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kama tunaipenda migebuka basi tusichafue ziwa Tanganyika

Kama tunaipenda migebuka basi tusichafue ziwa Tanganyika

Pakua

Uchafuzi wa mazingira utokanao na viwanda katika miji kote duniani ni moja ya sababu kubwa zinazoathiri sekta ya kilimo na uvuvi ambapo viumbe wa baharini, mito na hata maziwa wamekuwa katika hatari ya  kutoweka.

Nchini Burundi, wavuvi na wakaazi wa kando ya ziwa wameanza kushuhudia athari za uharibifuwa mazingira katika ziwa Tanganyika ambako aina ya samaki maarufu wajulikanao kama migebuka au mikeke wameanza kutoweka miaka ya hivi karibuni, kisa uchafuzi wa ziwa utokanao na viwanda kueklekeza maji taka yaliyojaa sumu kwenye ziwa hilo.

Mwandishi wetu wa maziwa makuu, Ramadhani kibuga ametembelewa mwaloni na kuzungumza na baadhi ya wavuvi na wananchi ili kupata maoni yao kuhusu janga hilo. Ungana naye katika Makala hii.

Audio Credit
Patrick Newman/ Ramadhani Kibuga
Audio Duration
5'3"
Photo Credit
UN Photo.