Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Warohingya wataka hakikisho la usalama kabla ya kurejea

Warohingya wataka hakikisho la usalama kabla ya kurejea

Pakua

Mpaka sasa wakimbizi wa Rohingya waliosaka hifadhi huko Bangladesh bado hawajaona dalili yoyote njema ya kuwawezesha kurejea nyumbani kwa hiari.

Naibu Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kibinadamu, OCHA Ursula Mueller amesema hayo leo jijini New York, Marekani akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa baada ya ziara yake ya siku sita nchini Myanmar.

Amesema wakimbizi hao walimweleza madhila wanayokumbana nayo nchini mwao kwenye jimbo la Rakhine ikiwemo ukosefu wa usalama na pia kuzuia kupata huduma kama vile za afya na elimu, na zaidi ya yote..

(Sauti ya Ursula Mueller)

“Hata hali ndani ya kambi ni mbaya sana. Kwa hiyo kile ambacho kingalikuwa ishara kwa wakimbizi walioko Bangladesh ni hali kuwa bora ndani ya kambi na pia kushughulikia maridhiano na maendeleo.”

Alipoulizwa kuhusu mazungumzo yake na Kiongozi na mshauri mkuu wa serikali ya Mynmar Aung Sun Suu Kyi kuhusu mustakhbali wa warohingya takribani 700,000 waliokimbia nchi hiyo pamoja na wengine 400,000 waliosalia jimbo la Rakhine, Bi.Mueller amesema..

(Sauti ya Ursula Mueller)

Alitaja kuwa kipaumbele cha malengo yake ni kusaka maridhiano ya kijamii na amani ya ndani na kwamba serikali itajikita katika jimbo la Rakhine ambalo ni moja ya majimbo maskini zaidi Mynamar.”

Audio Credit
Siraj Kalyango
Audio Duration
1'29"
Photo Credit
© UNHCR / Andrew McConnell