Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ulemavu hautuzuii kubadili maisha yetu

Ulemavu hautuzuii kubadili maisha yetu

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wakimbizi kutoka Burundi ambao waliamini kuwa maisha yao yatazidi kuwa duni kutokana na ulemavu, sasa nuru imeanza kuwaangazia baada ya kutumia stadi na maarifa yao kuboresha maisha. 

Nats.

Katika kambi ya wakimbizi ya Lusenda, jimboni Kivu Kusini nchini DRC,  wakimbizi 32 wanawake na wanaume kutoka Burundi ambao wote wana ulemavu wamechukua hatua ya kijasiri.

Wamepuuza fikra potofu ya kwamba ulemavu ni kukosa uwezo. Miongoni mwao ni Mathias Nzorigendera ambaye ubaguzi uliwapa machungu.

(Sauti ya Mathias Nzorigendera)

Na ndipo wakachukua hatua ya kuunda kikundi kiitwacho Dufashanye yaani tusaidiane kwa kirundi na kufungua karakana ya kutumia vyuma chakavu kutengeneza sufuria, sahani, birika na pasi za mkaa.

(Sauti ya Mathias Nzorigendera)

Vyombo  hivyo vinauzwa kwenye soko lililopo kambini Lusenda. Pamoja na kupata usaidizi kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Dufashanye wana ndoto zaidi.

(Sauti ya Mathias Nzorigendera)

 

Pakua
Audio Credit
John Kibego
Audio Duration
1'42"
Photo Credit
Picha ya UN