Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nishati ya jua yaleta nuru kwenye umwagiliaji mazao

Nishati ya jua yaleta nuru kwenye umwagiliaji mazao

Pakua

Mitambo ya umwagiliaji maji inayotumia nishati ya jua imekuwa muarobaini siyo tu katika kuimarisha lishe na kuongeza kipato bali pia kupunguza makali ya mabadiliko ya tabianchi.

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema hayo kwenye ripoti yake iliyochapishwa hii leo ikisema kuwa nchi za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ni wanufaika.

Olcay Unver ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa FAO akisimamia kitengo cha ardhi na maji ametaja faida za mitambo hiyo kuwa ni …

(Sauti ya Olcay Unver)

“Hakuna hewa chafuzi kwenye uzalishaji wa nishati ya jua, hiyo inapunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. Pia kuna faida ya kuhimili mabadiliko kwa kuwa wakulima wanatumia maji kutoka ardhini badala ya maji waliyohifadhi kutokana na mvua au kwingineko.”

Hata hivyo FAO inasema pamoja na faida hizo na kwamba mitambo hiyo ni rahisi ni lazima kuwepo kwa utaratibu wa usimamizi kwa sababu..

(Sauti ya Olcay Unver)

“Umwagiliaji kwa njia ya nishati ya jua hausimamiwi na serikali kuu kwa hiyo ni vigumu kudhibiti na kusimamia,  hivyo iwapo suala la uwezo wa mifumo ya mitambo hiyo halitazingatiwa sambamba na kanuni zake, kuna hatari ya maji kutumika kupita kiasi na ndio maana tunasisitiza kuanzishwa kwa mfumo mkuu wa usimamizi hasa kwenye uendelezaji wa uwezo wa mitambo hiyo.”

Ni kwa mantiki hiyo amesema FAO imeanzisha mwongozo ambao unazingatia..

(Sauti ya Olcay Unver)

“Mahitaji ya maji, masuala ya fedha na kuangazia faida zitokanazo na matumizi yake shambani na kushauri wakulima juu ya mfumo bora zaidi na pia katika kuunda mfumo wa umwagiliaji na matunzo ya mitambo hiyo.”

Audio Credit
Flora Nducha
Sauti
1'44"
Photo Credit
IFAD/Video Capture