Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Elimu kwa mtoto wa kike kwa jamii za wafugaji bado ni mtihani

Elimu kwa mtoto wa kike kwa jamii za wafugaji bado ni mtihani

Pakua

Mbali ya mila na desturi, mazingira na mazoea vimetajwa kuwa chachu ya kumkosesha elimu mtoto wa jamii za wafugaji nchini Tanzania kama Wamaasai na Wamang’ati.

Ingawa elimu inatajwa kuwa ni ufunguo wa maisha , lakini sio kwa wote nchini Tanzania na hususani katika jamii za wafugaji hasa wa Kimaasai na Kimang’ati, ambako kwa miaka nenda miaka rudi jamii hizo  zimejikita ktika ufugaji na hasa wa kuhamahama hali inayofanya kuwa vigumu watoto wengi kwenda shule , lakini kwa watotowakike changamotoni kubwa zaidi kwani mila zinamuuona kama asiye na thamani, lakinipia nafasi yake kubwa ipo katika malezi ya familia na jikoni.

Juhudi kubwa zinaendelea kufanyika nchini humo na serikali, wanaharakati na hata mashirika ya Umoja wa Mataila likiwemo la kuhudumia watoto UNICEF kuhakikisha haki ya elimu kwa jamii hizo inatambulika lakini bado kuna changamoto kubwa.

John Kabambala kutoka Radio washirika Tanzania Kidstime amezitembelea baadhi jamii hizo mkoani Pwani ili kupata maoani ya vijana kuhusu elimu. Akianza na Moi Loita kutoka katika jamii ya Kimasaai aliyebahatika kupata elimu

(SAUTI YA MOI LOITA)

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
2'7"
Photo Credit
Haki ya kuendelezwa inajumuisha pia watoto wote awe wa kike au wa kiume kupata elimu ya msingi na hapa ni Tanzania watoto wakiwa darasani. (Picha:UNICEFTZ Facebook)