Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma ya afya kwa wote ni zaidi ya kuwa na bima

Huduma ya afya kwa wote ni zaidi ya kuwa na bima

Pakua

Shirika hilo limesema kuna baadhi ya nchi zimepiga hatua kubwa katika kuelekea utimizaji wa lengo la afya kwa wote kwa kuzingatia ajenda ya maendeleo endelevu au SDGs ya mwaka 2030, lakini bado nusu ya watu wote duniani hawawezi kumudu kupata huduma za afya wanazohitaji.

Katika ujumbe wake wa siku ya afya duniani itakayoadhimishwa kesho Aprili 7, mkurugenzi mkuu wa WHO Dr. Tedros Gabreyesus amesema endapo nchi zitataka kutimiza lengo la afya hapo 2030 basi itabidi watu bilioni moja wafaidike na huduma ya afya kwa wote (UHC) ifikapo mwaka 2023, lasivyo lengo hilo halitotimia.

Amesisitiza kuwa hakuna mtu anayestahili kuchagua kati ya kununua dawa au kununua chakula, naye Dr. Hillary Kipruto wa WHO nchini Kenya amekumbusha kwamba huduma kwa wote si kitu kimoja

(Sauti ya Dkt. Hillary Kipruto)

Na hivyo ameshauri..

(Sauti ya Dkt. Hillary Kipruto)

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
1'38"
Photo Credit
Wafanyakazi wa IOM wanatoa huduma za dharura na huduma za afya kwa watu wa Rohingya na wenyeji. Picha: (IOM) 2017