Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amchoropoka ngariba na sasa apaza sauti kupinga FGM

Amchoropoka ngariba na sasa apaza sauti kupinga FGM

Pakua

Harakati za kuondokana na ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake , FGM, zinazaa matunda pale msichana anapopaza sauti na jamii yake kuitikia.

Hiyo imekuwa dhahiri kwa Purity Soinato Oiyie, msichana wa kimasai kutoka Kenya ambaye akiwa na umri wa miaka 11 alikwepa kitendo hicho haramu.

Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, Purity amesimulia alifanikiwa vipi kukwepa mkono wa ngariba.

(Sauti ya Purity Soinato Oiyie)

Hivi sasa Purity mwenye umri wa miaka 22 amefanikiwa kuhitimu shahada yake ya kwanza ya Chuo Kikuu akijikita katika masuala ya elimu. Pamoja na kwamba ni mjumbe wa Bodi ya kitaifa nchini Kenya ya kukabiliana na FGM, Purity hutumia muda wake mwingi kuhamasisha wasichana na jamii dhidi ya , ukeketaji. Je mwitiki uko vipi?

(Sauti ya Purity Soinato Oiyie)

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
1'19"
Photo Credit
Wanawake wa katika kijiji cha Kiltamany nchini Kenya wanaopinga FGM katika jamii yao.(Picha:UNICEF/UN08769/Leadismo)