Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji watarajie nini kutoka Brussels?

Wahamiaji watarajie nini kutoka Brussels?

Sintofahamu hiyo ni pamoja na masuala ya ulinzi kwa wahamiaji walio hatarini zaidi kama wanawake, watoto na wazee, usimamizi bora wa mienendeo ya wahamiaji pamoja na makubaliano ya kimataifa kuhusu uhamiaji.

Mepama, Mkurugenzi Mkuu wa IOM William Lacy Swing amekaribisha kuendelea kwa mazungumzo ya kimkakati kati ya shirika lake na EU hususan wakati huu ambapo changamoto za uhamiaji na fursa zake zinaibua mijadala ya kisiasa na kushika nafasi ya juu katika ajenda za Ulaya na kimataifa.

Amesema huu ni wakati muafaka wa kuwa kitu kimoja katika kuainisha sera ya uhamiaji kimataifa kwa kuwa hoja zinazogonga vichwa vya watu kuhusu uhamiaji zinamgusa kila mtu kuanzia nchi tajiri, maskini hadi wahamiaji wenyewe walio hatarini.

Bwana Swing amesema fursa hii ya kihistoria itatoa mwanya wa kujenga mfumo ambamo kwao watu wataweza kusafiri kwa usalama, kihalali na bila shinikizo huku haki zao za msingi zikilindwa.

Mkutano huu ni wa tano wa aina yake kati ya IOM na EU tangu kuanza kwa ushirikiano wa kimkakati kati ya pande mbili hizo mwaka 2012.

 

Pakua
Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
1'20"
Photo Credit
Picha ya UNICEF/UNI199995/Gilbertson V