Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfumo wa chakula enedelevu ndio muarobaini wa SGDs 2030: Graziano

Kongamano la kimataifa la siku tatu kujadili uzalishaji na uhakika wa chakula duniani linaendelea leo mjini Roma Italia. John Kibego na taarifa kamili

(TAARIFA YA KIBEGO)

Kongamano hilo litakalomalizika April 5 limewaleta pamoja  zaidi ya washiriki  700 kutoka duniani kote, wakiwemo wataalamu wa masuala ya chakula, asasi za kiraia, vyongozi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali mbalimbali, ili kujadili mbinu na mikakati endelevu za uzalishaji na uhakika wa chakula duniani.

ZMkurugenzi mkuu wa shirika la chakula na kilimo FAO ambao ndio waandaaji wa kongamano hilo , Graziano da Silva ametoa wito  kwa mashirika ya kibinadamu kuwekeza katika mifumo itakayozalisha chakula kinachozingatia afya bora kwa jamii zote duniani.

 (Sauti ya Graziano)

Tunahitaji kuzingatia na pia kubadili namna tunayozalisha na kula chakula. Tunahitaji kuweka mifumo ya chakula endelevu ambayo hutoa chakula chenye afya na lishe bora , na pia kuhifadhi mazingira. Kilimo cha kisasa kinaweza kutoa mchango mkubwa katika mchakato huu. "

Naye Gilbert F.Houngbo ambaye ni mkurugenzi wa mfuko wa kimataifa wa ufadhili wa maendeleo ya kilimo IFAD akisisitiza hoja hiyo amesema 

(Sauti ya Gilbert F.Houngbo)

"Kazi yetu katika siku chache zijazo ni kubwa lakini muhimu, kufanya mabadiliko makubwa katika njia tunayotumia katika uzalishaji wa kilimo ili iwe  endelevu na imara."

Kongamono hili nimwedelezo wa lile la mwaka 2014, la mataifa ya kusini mwa Amerika na la  2015 lililohusisha nchi za kusini mwa Afrika.

Mpaka sasa wataalum 1400  wameshiriki mchakato huu kutoka  nchi 170, washirika katika mpango wa kimatataifa wa kupiga vita tatizo la njaa kwa kutafuta njia mbadala za uzalishaji na kuhakikisha uhakika wa chakula duniani.

Pakua

 Sauti ya Graziano)

Audio Credit
John Kibego
Audio Duration
1'42"
Photo Credit
Picha ya FAO/Tibasaaga