Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kazi ya kupokonya silaha si rahisi-UN

Kazi ya kupokonya silaha si rahisi-UN

Kamati ya upokonyaji silaha ya Umoja wa Mataifa imeanza leo vikao vyake vitakavyo jadilia upokoanyaji silaha ikiwemo za nyuklia na zile za maangamizi.

Akihutubia kikao cha ufunguzi Mkurgenzi na naibu mwakilishi wa ofisi ya  Umoja wa Mataifa inayohusika na upokonyaji silaha,Thomas Markram amesema ofisi yake inafanya juu chini kutimiza suala hilo la upokonyaji wa silaha na kuongeza kuwa

(SAUTI YA MARKRAM)

Imekuwa ikitayarisha mwelekeo wenye mkakati unaowajumuisha wote katika kuunda ajenda hii na tunafanya kila juhudi kuweza kutoa mwelekeo huo katika majira ya chipukizi”.

Mkutano huu umekuja siku chache baada ya katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress kuonyesha wasiwasi wake kuhusu mvutano kati ya Urusi na Marekani, mataifa mawili yenye nguzu za silaha za maangamizi.

Pia katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ameelezea hofu yake ya  mwelekeo wa mvutano huo kufanana kidogo na zama za vita baridi kati ya Marekani na Urusi lakini wakazi wa zama hizo pande mbili hizo zilikuwa na udhibiti wa mvutano huo.

Pia tisho lingine ni matamashi ya pande husika katika rasi ya Korea ambapo bwana Markram amesema

(SAUTI YA MARKRAM)

Miezi sita iliyopita, katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alilionya baraza la usalama kuhusu tisho la matumizi ya Nuklia. Alitiwa wasiwasi na matamshi ya ugomvi katika rasi ya Korea jambo ambalo lilikuwa linaivuta hali kama kuelekea kwenye mgogoro.”

Licha ya hali kuwa ya wasiwasi kwa upande mwingine amesema kuwa kumekuwepo na ishara za maendeleo fulani ambapo shirika hilo linaweza kusaidia kutoa muongozo

Pakua

Akihutubia kikao cha ufunguzi Mkurgenzi na naibu mwakilishi wa ofisi ya  Umoja wa Mataifa inayohusika na upokonyaji silaha,Thomas Markram amesema ofisi yake inafanya juu chini kutimiza suala hilo la upokonyaji wa silaha 

Audio Credit
Siraj Kalyango
Audio Duration
1'48"
Photo Credit
Picha ya UN/Elma Okic