Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume ya uchaguzi Afghanistan mnafanya kazi nzuri: UN

Tume ya uchaguzi Afghanistan mnafanya kazi nzuri: UN

Pakua

Umoja wa Mataifa umepongeza na kukaribisha hatua zilizopigwa na tume huru ya uchaguzi nchini Afghanistan (IEC) kwa kupanga Oktoba 2018 kufanyika uchaguzi wa bunge na madiwani.

Akizungumzia hatua hiyo mkuu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNAMA na mwakilsihi maalumu wa Katibu Mkuu bwana Tadamichi Yamamoto amesema kuweka tarehe rasmi ya uchaguzi ni hatua chanya na muhimu katika kazi za IEC.

Ameongeza kuwa uchaguzi huru, wa wazi na utakaojumuisha pande zote ni kiungo muhimu kwa Afghanistan kuonyesha uimara na ukomavu katika mchakato wa kisiasa wa demokrasia.

Yamamoto amehimiza kuwa ushiriki wa Waafghanistan wote kwatika mchakato wa uchaguzi sio tu katika upigaji kura peke yake,  ni wa lazima na chachu ya mafanikio ya amani.

Desemba mwaka 2017 wahisani waliahidi kufadhili hadi asilimia 90 ya dola milioni 28.4 zinazohitajika katika bajeti ya uandikishaji wapiga kura na pia ahadi zaidi za kusaidia tume ya uchaguzi IEC na tume ya malalamiko ya uchaguzi ECC.

Pia Yamamoto amekumbusha kuwa Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa bado wamedhamiria kuisaidia Afghanistan katika mchakato wao wa uchaguzi.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
1'13"
Photo Credit
Fraidoon Poya / UNAMA