Furaha itarejea Yemen tukiwekeza kwa watoto- UNICEF

26 Machi 2018

Miongoni mwa mashambulizi hayo ni yale ya Jumapili jioni yaliyoelekezwa kwenye miji ya Saudi Arabia ikiwemo Riyadhi, mashambulizi ambayo  kikundi cha wahouthi kimekubali kuhusika nalo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali mashambulizi hayo akiendelea kusisitiza kuwa operesheni za kijeshi katu hazitomaliza mzozo wa Yemen.

Amezitaka pande zote kuzingatiwa wajibu wao kwa mujibu wa sheria za kibinadamu za kimataifa zinazotaka mashambulizi yoyote yale yasilenge raia au miundombinu ya kiraia kama vile hospitali na shule.

Wakati huo huo, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Geert Cappalaere amehitimisha ziara yake nchini Yemen akielezea jinsi vita nchini humo vinadumaza maendeleo ya watoto wa kike na wa kiume milioni 11.

(Sauti ya Geert Cappalaere)

“Miaka mitatu ya vita nchini Yemen imesababisha utapiamlo uliokithiri kuongezeka maradufu zaidi. Mwaka 2015 watoto 200,000 walikuwa na utapiamlo. Hii leo kwa sababu ya vita vilivyodumu miaka mitatu, idadi imeongezeka maradufu na kufanya pengine Yemen iwe nchi ya kwanza kati ya tatu duniani zenye idadi kubwa ya watoto wenye utapiamlo uliokithiri.”

Bwana Cappalaere ametaja sababu za utapiamlo kuendelea kukithiri miongoni mwa watoto nchini Yemen kuwa ni pamoja na

(Sauti ya Geert Cappalaere)

“Tishio la njaa kali bado lipo nchini Yemen. Shida ya maji safi ya kunywa bado imesalia nchini Yemen.”

Mkuu huyo wa UNICEF kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini akatoa wito..

(Sauti ya Geert Cappalaere)

“Jukumu la kwanza ni rahisi, vita hivi katili dhidi ya watoto lazima vikome, si kesho bali leo. Pili kwa niaba ya watoto mamilioni ya watoto wa kike na wa kiume wa Yemen ni jambo rahisi kabisa. Natoa wito kwa mamlaka nchini kote kuwezesha misaada ya kibinadamu kuwasilishwa bila masharti yoyote.”

Bwana Cappalaere ameseam awali Yemen ilitambulika kama Arabia Felix au eneo la uarabuni lenye furaha, lakini hivi sasa furaha imetoweka.

Amesema furaha itarejea Yemen pale tu jamii ya kimataifa itawekeza kwa watoto na badala ya kuwekeza kwenye vita, iwekeze kwenye elimu.

 

Audio Credit:
Assumpta Massoi
Audio Duration:
2'26"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud