Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sualala uhamiaji si la mtu mmoja:UM

Sualala uhamiaji si la mtu mmoja:UM

Pakua

Suala la uhamiaji ni mtambuka na sio la kushughulikiwa na mtu mmoja au taifa moja, linahitaji mshikanao wa kimataifa kulipatia ufumbuzi.

Hayo yamesemwa na William Lacy swing, mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la uhamiaji IOM, akifungua mjadala wa kimataifa wa siku mbili mjini New York Marekani kuhusu ushirika bunifu na jumuishi kwa ajili ya kushughilikia suala la kimataifa la uhamiaji na kutaja mambo matatu muhimu

(SAUTI YA SWING)

Mosi majadiliano bado yanaendelea , na mkakati wenyewe unasisitiza umuhimu wa ushirika , pili tunahitaji kutoa msaada wa kiufundi , rasilimali na ushirika unaohitajika ili kushughulikia uhamiaji, na tatu tunayo ajenda ya 2030 inatotoa wito wa ujumuishwaji na ushirika wa uhamiaji.”

Na kuhusu suala la wafanyakazi wahamiaji wa nyumbani ambao pasi zao za kusafiri mara nyingi hukamatwa au kushilkiliwa na waajiri wao mbunge kutoka County ya Kiambuu nchini  Kenya,  Jude Njomo alieshiriki mkutano wa jumuiya ya mabunge duniani kuhusu suala hilo la uhamiaji anasema

(SAUTI YA JUDE NJOMO

Mjadala huo umeyaleta pamoja mashirika na wadau mbalimbali  mkiwemo mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto  , UNICEF na shirika la kazi duniani ILO .

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
1'37"
Photo Credit
UN News/Patrick Newman