Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yagawa mashine za kisasa za kupima TB kwa hospitali binafsi

Tanzania yagawa mashine za kisasa za kupima TB kwa hospitali binafsi

Pakua

Kuelekea siku ya kimataifa ya kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu, TB duniani hapo kesho, Tanzania imesema imeongeza idadi ya mashine za kisasa za kupima makohozi ya wahisiwa wa TB kutoka 66 mwaka 2015 hadi 186 mwezi huu wa Machi. Selina Jerobon na maelezo zaidi.

Waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dodoma hii leo ametaja sababu za kuanza kutumia mashine hizo ziitwazo GeneXpert badala ya X-Ray iliyozoeleka.

(Sauti ya Ummy Mwalimu)

Amesema mashine hizo zenye thamani ya shilingi milioni 38 kwa kila moja zimesambazwa pia katika hospitali binafsi na wameanzia na zile zilizoko mkoani Dar es salaam ambazo ni  Kairuki, Hindu Mandal, Agakhan, TMJ na Regency.

Waziri huyo wa afya pia ametangaza kuwa sasa Tanzania ina dawa ya TB kwa watoto, jambo alilosema linamtia moyo zaidi.

(Sauti ya Ummy Mwalimu)

Audio Credit
Selina Jerobon
Audio Duration
1'37"
Photo Credit
Watendaji wa mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma nchini Tanzania, NTLP wakifuatilia usimamizi wa dawa kwenye moja ya maduka ya dawa muhimu chini ya Mpango wa ADDO. Pichani mtendaji akikagua fomu anayopatiwa mgonjwa anapatiwa mtu anayehisiwa kuwa na ug