Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sisi ni warendile tutambulike tulivyo: Alice

Sisi ni warendile tutambulike tulivyo: Alice

Pakua

Yaelezwa kuwa utamaduni ni kielelezo cha ustawi wa kila jamii. Utamaduni hudhihirishwa kwa njia mbalimbali iwe lugha, mila, mavazi, chakula na kadha wa kadha. Kutotambulika kwa utamaduni wa mtu au jamii ina maana ni kutokomea kwa jamii hiyo na ndio maana jamii ya warendile walioko kaunti ya Marsbit nchini Kenya wanapaza sauti ili kabili hilo litambuliwe kwa kina ili hata mila zao basi ambazo si potofu ziweze kutumiwa katika kusongesha maisha si tu kwenye jamii zao bali pia kwingineko ambako zinafaa.

Alice Lesepen, mwanaharakati kutoka jamii ya warendile, alikuwepo New  York, Marekani kushiriki vikao vya kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW na vingine vilivyoitishwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wanawake, UNWomen. Kando mwa vikao hivyo aliieleza Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kile anachotaka kuhusu ustawi wa kabila lao. Kwa kina basi ungana na Flora Nducha.

 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
3'48"
Photo Credit
UN News/Assumpta Massoi