Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uzee haukwepeki ni safari ya kila mmoja:UN

Uzee haukwepeki ni safari ya kila mmoja:UN

Mtaalam  huru wa Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya Georgia kuweka kipaumbele cha mkakati wa  kuwajumuisha wazee na pia kuzingatia usawa wa watu hao.

Rosa Kornfeld-Matte, mtaalamu huru kuhusu masuala ya wazee kufurahia haki zote za binadamu ametoka wito huo wakati akikamilisha ziara yake ya kwanza rasmi nchini Georgia.

 Nchi hiyo, kwa mujibu wa sensa ya watu iliyopita, inasemekana kuwa na idadi kubwa ya watu waliokula chumvi nyingi ,yaani wazee, katika eneo la Kaukasia kusini, ambapo ilionyesha kila mtu mmoja kati ya watano ana umri  wa miaka 60 au zaidi. Taarifa inasema hii ina maanisha kuwa ifikapo mwaka wa 2050, asilimia ya waliona umri zaidi ya miaka 60 itaongezeka kwa zaidi ya asilimia 30.

Kornfeld-Matte amesema kuna taarifa mbalimbali  za unyanyasaji wa wazee  ukifanywa na watu tofauti wakiwemo hata  watu wa familia na wanaowahudumia.

Ameiomba serikali ya nchi hiyo kuja na mbinu mpya  za kuzuia vitendo hivyo. Pia amekaribisha  hatua ya serikali ya Georgia, ya hivi majuzi, ya kukubali mpango tekelezi wa kitaifa wa kufanikisha   sera ya serikali kuhusu idadi ya watu wanaozeeka kama hatua moja iliokuwa inasubiriwa kwa hamu  kuelekea kuboresha mfumo wa kuwasaidia wazee.

Pakua

Mtaalam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu wazee kufurahia kikamilifu haki zao za binadamu Rosa Kornfeld-Matte amesema kuwa taifa la Georgia lina idadi kubwa ya wazee yaani watu  wa umri wa miaka 60 na kwenda juu. Pia    kusema kuwa idadi kubwa ya wazee inateswa ,hivyo kuiomba serikali ya Tiblis, kuwahusisha wazee kwani uzee si ugonjwa.

Audio Credit
Siraj Kalyango
Audio Duration
1'23"
Photo Credit
Picha ya UN/Jean-Marc Ferré