Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pale Mmaasai mwanaume anapopigia chepuo haki za wamasai wanawake

Pale Mmaasai mwanaume anapopigia chepuo haki za wamasai wanawake

Pakua

Ni kawaida kwa mtu anayeamua kusimama kidete dhidi ya mila zinazopigiwa chepuo na wenzake kukumbwa na misukosuko! Na ni misukosuko zaidi pindi mtu huyo ni wa kabila la kimasai na ni mwanaume anayetetea haki za wamasai wanawake na wasichana wanaokumbana na mila potofu kama vile ukeketeji na kupokwa ardhi zao pindi mume anapofariki dunia. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa Alais Esoto, mratibu wa shirika la kiraia la Naserian huko Monduli mkoani Arusha nchini Tanzania. Alikumbana na mengi lakini hakukata tamaa na sasa ameona matunda. Bwana Esoto yuko New York, Marekani akihudhuria mkutano wa 62 wa hali ya wanawake duniani na kando mwa mkutano huo amezungumza na Assumpta Massoi wa Idhaa hii kuhusu hali ilivyo hivi sasa baada ya harakati zake. Lakini kwanza anaanza kwa kuelezea changamoto aliyokutana nayo na aliikabili vipi.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
4'22"
Photo Credit
Maasai, watu wa asili ya Kenya barani Afrika. Picha: UM