Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muziki wabadili mtazamo wa wakimbizi wa CAR

Muziki wabadili mtazamo wa wakimbizi wa CAR

Pakua

Tangu mwaka 2013, mamia ya maelfu ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR wamelazimika kukimbia makazi yao kufuatia vurugu na mauaji ya kikatili yanayotekelezwa na wapiganaji nchini humo.  Watu zaidi ya 180,000 wamekimbilia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, moja ya nchi zilizo masikini zaidi duniani.

Kupitia mfululizo wa warsha za mafunzo ya ngoma na muziki, mradi wa "Refugees on the move au Wakimbizi katika harakati," unaowezeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na mashirika yasiyo ya kiserikali ya “Wasanii kwa ajili ya Maendeleo”, una lengo la kupunguza unyanyasaji katika kambi za wakimbizi na kusaidia wakimbizi kuunda uhusiano wa kijamii.

Fabrice Don de Dieu, msanii wa kupanga miondoko ya dansi pamoja na kampuni yake ya wanamuziki na wacheza ngoma, "Kongo Drama" wamepeleka ngoma na muziki kwa baadhi ya wakimbizi katika jimbo  la ubangi nchini DRC.  Je, kulikoni? Ungana na Selina Jerobon katika makala hii...

Audio Credit
Selina Jerobon
Audio Duration
3'56"
Photo Credit
Picha: UM/Video capture