Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukinzani wa sheria ni kikwazo cha umiliki ardhi miongoni mwa wanawake Tanzania- LANDESA

Ukinzani wa sheria ni kikwazo cha umiliki ardhi miongoni mwa wanawake Tanzania- LANDESA

Pakua

Mkutano wa 62 wa hali ya wanawake duniani, CSW62 ukiendelea kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini  New York, Marekani, hoja ya umiliki ardhi imetamalaki miongoni mwa washiriki. Wawakilishi wa wanawake na wasichana wa vijijini pamoja na wanawake wenyewe wanabadilishana uzoefu juu ya kile cha kufanya ili kuhakikisha kuwa umiliki wa ardhi unafanyika bila kujali jinsia ya mtu. Mathalani nchini Tanzania tumetaka kufahamu hali iko vipi ambapo Assumpta Massoi amezungumza na mmoja wa washiriki, Monica Mhoja ambaye ni mkurugenzi mkazi wa shirika la kutetea umiliki kamilifu wa ardhi, LANDESA tawi la Tanzania. Bi. Mhoja anaanza kwa kuelezea hali ya umiliki ardhi nchini humo.

 

LANDESA, CSW62, Monica Mhoja, Tanzania

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
3'49"
Photo Credit
UN News/Flora Nducha