Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usawa wa kijinsia ndio mkatakati wangu-Guterres

Usawa wa kijinsia ndio mkatakati wangu-Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuwa uongozi wake unatilia mkazo usawa wa kijinsia katika ngazi zote husasan za Umoja wa Mataifa.

Katibu Mkuu ameyasema hayo leo mjini New York wakati anakutana na makundi ya kiraia -Civil Society-pembezoni mwa mkutano wa kamisheni ya hali ya wanawake dunaini,CSW62  unaoendelelea  ambao unagusia mitizamo mbalimbali kutoka kwa washiriki.

 Ametoa mfano wa mgawanyo wa kijinsia katika ngazi mbalimbali za uongozi katika baraza hilo ambalo wakati alipochukua hatamu  amesema wanaume walikuwa asili mia 60 ilhali wanawake asili mia 40 na kueleza hali ilivyo kwa sasa.

(SAUTI YA GUTERRES )

“Sasa, badala ya asili mia 60 ya wanaume na asili mia 40 ya wanawake tuna  asili mia 56 ya wanawake asili mia 44 ya wanaume”…

Pia amesema kuwa shabaha yake nyingine kuu ni kupiga vita unyanyasaji wa kingono wa   mashirika ya Umoja wa Mataifa dhidi ya watu wa nje.

(SAUTI YA GUTERRES )

“ Hii ni shida iliyoko katika vikosi vya kulinda amani na  pia  katika mashirika mengine ya utoaji misaada ilioko mashinani”

Hata hivyo amesema  wanafanya kila liwezekanalo kuweza kuondoa tatizo hilo japo será ya kutovumilia visa hivyo ilitangazwa mda mrefu uliopita ,tatizo  kwa  sasa amesema ni utekelezaji.

Pakua
Audio Credit
Siraj Kalyango
Audio Duration
1'30"
Photo Credit
UN Photo/Loey Felipe