Wanaharakati wa mazingira mjini nchini Burundi wameanza kampeni ya upandaji wa miti na mauwa kwenye barabara muhimu za jiji la Bujumbura. Shughuli hiyo inanuwia kung’arisha jiji hilo na kuandaa jiji kwa kuzingatia swala la mazingira na mabadiliko ya tabia nchi. Maelefu ya miche ya miti na mauwa yatapandwa katika kampeni hiyo ya kimazingira itakayodumu wiki mbili.