Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashambulio haya ni lazima yajibiwe- Zeid

Mashambulio haya ni lazima yajibiwe- Zeid

Kamishna mkuu wa haki za binadamu, Zeid Ra’ad Al Hussein amekemea  hatua za utawala wa Ufilipino za kumuweka katika orodha ya magaidi, muwakilishi  maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu asili, Victoria Tauli-Corpuz na kusema  kitendo hicho  hakikubaliki na kusema ni lazima lijibiwe.

(Sauti ya zeid victoria)

“Bila shaka hii haiwezi kukubalika dhidi ya  muwakilishi maalum akifanya kazi kwa niaba ya jamii ya kimaaifa ambae ujuzi wake unahitajika mno na bazala la haki za binadamu kufanyiwa hivyo.”

Akimnukuu mwakilishi mwenye akisem akuwa huenda hatua hiyo imechochewa na mhatua yake ya kukaripia uawala dhidi ya mauaji ya kiholela kwa wanaodaiwa kuw a wanajihusisha na madawa ya kulevya vita alivyoanza kiongozi wa sasa wa Ufilipino.

Victoria na wenzake wanalaumiwa kuwa wanachama wa vyama vya  cha Kikomunist cha CCP pamoja na New Peoples Army-NPA.

Pia majuzi inadaiwa kuwa rais wa sasa wa Ufilipino  alidaiwa kutumia maneno yasiyofaa kumuhusu Muwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu asili. Hilo nalo kamishna Zeid alilishutumu.

(SAUTI YA ZEID UFILIPINO)

“Matamshi kama haya kwa kweli hayakubaliki…hayakubaliki.

Ameongeza kuwa kiongozi huyo anafaa kuchunguzwa  na wataaalamu wa masuala ya akili.

Pakua
Audio Credit
Siraj Kalyango
Sauti
1'29"
Photo Credit
Picha ya UN/JC McIlwaine