Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati ni sasa wa kumuinua mwanamke wa kijijini: Sudan Kusini

Wakati ni sasa wa kumuinua mwanamke wa kijijini: Sudan Kusini

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yamefanyika juma hili kila kona ya dunia. Kauli mbiu ikiwa “Wakati ni sasa wa kumuinua na mkomboa mwanamke wa kijijini”

Huko Sudan Kusini maadhimisho yaliambatana na burudani ya ngoma za asili na ujumbe wa kudumisha amani  na hasa ulinzi na usalama kwa kuwashirikisha zaidi wanawake ambao ni waathirika wakubwa wa machafuko.

Watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, wanaharakati wa haki za wanawake, na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia mkuu wa mpangu wa Umoja huo nchini Sudan Kusini David Shearer hakukosa. Basi ungana na Flora Nducha katika makala hii ujue mambo yalivyojiri

 

Pakua
Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
3'45"
Photo Credit
Wanawake Sudan Kusini.Picha:Radio Miraya