Umoja wa Mataifa unakazia michezo kwa maendeleo iwe kwa vijana au wazee, wanawake au wanaume, wasichana au wavulana. Michezo ni mojawapo ya mambo yanayosaidia kumwezesha binadamu kustawi iwe ni kwa kupata ajira kupitia michezo au kuimarisha viungo vyake na wakati mwingine ni burudani. Ni kwa miongoni mwa misingi hiyo, wasichana wakimbizi kutoka Burundi walioko ukimbizini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wameamua kucheza soka na ndoto yao ni kwamba iko siku watacheza viwanja vya kimataifa kama ilivyo akina Suarez! Kwa kina basi kuhusu ndoto zao hizo ungana na Assumpta Massoi kwenye makala hii.