Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

EU yatoa euro milioni 115 kuwarejesha nyumbani wahamiaji 16, 000: IOM/UNHCR

EU yatoa euro milioni 115 kuwarejesha nyumbani wahamiaji 16, 000: IOM/UNHCR

Mashirika ya Umoja wa Mataifa, likiwemo lile la uhamiaji IOM na lile la kuhudumia wakimbizi UNHCR, yameanza zowezi la usafirishaji wa wakimbizi 16,000 kuturudi makwako kupitia mpango wa  wakimbizi kurudi kwa hiari, na kuanzisha shughuli za kimaendeleo ili kujikwamua na maisha.

Mpango huo wa krudi nyumbani kwa hiari uliotanganzwa rasmi na viongozi kutoka UNHCR, ambaye ni kamishina mkuu wa wakimbizi Bwana Turk, mkurugenzi mkuu wa IOM William Lacy Swing, na mjumbe wa Muungano wa Afrika EL Fadil, ulitangazwa Desemba mwaka jana kwa msaada wa Muungano wa ulaya EU , Umoja wa Afrika AU na Umoja wa Mataifa tayari umefanikiwa kuwahamisha wakimbizi 3800,wanaohitaji ulinzi kutoka Libya na kwenda kwenye kambi ya mpito Chad, na wengine kupewa hifadhi ya kudumu katika nchi ya tatu.

EU, imetoa kiasi cha Euro milioni 115 ili kufanikisha zoezi hilo la kusafirisha wakimbizi wanaopewa hifadhi ya kudumu katika nchi ya tatu , na kuwawezesha  wale wanaorudi kwa hiari, kuanza maisha mapya punde wanapofika makwako.

Mwaka jana kupitia azimio la  Abidajan Umoja wa Mataifa, EU na AU waliweka bayana mikakati ya kuwawezesha wakimbizi kurudi kwa hiari na pia kutafutiwa hifadhi ya kudumu katika nchi ya tatu.

Pakua
Audio Credit
Selina Jerobon
Audio Duration
1'27"
Photo Credit
IOM Niger