Neno la Wiki: Kimanda
Katika Neno la Wiki hii leo tunaangazia neno “Kimanda” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.
Bwana Sigalla anasema Kimanda ni aina ya chakula, na inatumika zaidi katika yai iliyokorogwa na kukaangwa kwa kuchanganywa na nyanya, pilipili na vitunguu.