Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sheria itasaidia kudhibiti matumizi mabaya ya viuavijasumu: Dr Mbindyo

Sheria itasaidia kudhibiti matumizi mabaya ya viuavijasumu: Dr Mbindyo

Pakua

Shirika la afya ulimwenguni WHO linasema matumizi mabaya na ya kupindukia ya viuavijasumu au antibiotic yana athari kubwa sio tu kwa afya ya binadamu na wanyama bali pia katika uchumi. Sasa shirika hilo kwa kushirikiana na shirika la afya ya mifugo OIE wanazichagiza nchi kuchukua hatua ili kuepuka athari hizo kwa kudhibiti matumizi ya dawa za viuavijasumu kwa binadamu na wanyama. Dr Regina Mbindyo ni afisa wa madawa wa WHO nchini Kenya amezungumza na Flora Nducha wa idhaa hii kuhusu athari na jitihada zinazofanyika Kenya kudhibiti matumizi ya dawa hizo.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
3'49"
Photo Credit
Viuavijasumu,Picha na WHO