Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za binadamu si anasa- Guterres

Haki za binadamu si anasa- Guterres

Pakua

Akifungua kikao cha 37 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa huko Geneva, Uswisi hii leo, Bwana Guterres amesema ingawa tamko la haki za binadamu mwaka huu linatimiza miaka 70 bado haki hizo zinapuuzwa.

(Sauti ya Antonio Guterres)

“Lakini ni dhahiri kuwa maneno yaliyomo kwenye tamko hilo bado hayaendani na hali yalisi mashinani. Kivitendo, watu kote ulimwenguni bado wanakumbwa na vikwazo au hata wananyimwa haki zao za msingi. Usawa wa kijinsia unasalia hoja nzito, idadi ya wanawake na wasichana isiyofahamika wakikumbwa na ukosefu wa usalama, ghasia na haki zao kukiukwa.”

Amesema haki za binadamu si anasa, bali ni wajibu wa pamoja ambao nchi wanachama wameridhia kuzingatia.

Naye Kamishna Mkuu  wa haki za binadamu Zeid Ra’ad Al Hussein ametumia kuwanyooshea vidole wakiukaji wa haki akisema..

(Sauti ya Zeid Ra’ad Al Hussein)

“Hakuna tamaduni, sheria au dini inayounga mkono ukandamizaji. Mijadala kuhusu haki inaepukwa na wale wanaosaka kuipindisha kwa sababu ya kuhisi lawama, wale ambao wanaona aibu kuchukua uamuzi mgumu na wanufaika wa chambuzi zisizo na mashiko.”

 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
1'22"
Photo Credit
HRC(Picha ya UM/Jean-Marc Ferré)