Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuhifadhi na kupanua wigo wa misitu ni mtihani tunaotakiwa kushinda: FAO

Kuhifadhi na kupanua wigo wa misitu ni mtihani tunaotakiwa kushinda: FAO

Pakua

Idadi ya watu ikiendelea kuongezeka duniani na kutarajiwa kufikia bilioni 9 mwaka 2050, kuhifadhi na kupanua wigo wa mistu kwa ajili ya kuwezesha kuwalisha watu hawa imekuwa mtihani ambao dunia inapaswa kuushinda kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa . 

Hayo yamesemwa leo na shirika la chakula na kilimo FAO kwenye mkutano wa kimataifa wa siku tatu unaofanyika Roma Italia kwa lengo la kuchukua hatua za pamoja miongoni mwa sekta ili kukomesha ukataji miti na kupanua wigo wa misitu. Suala ambalo linahitaji utashi wa kisiasa na hatua madhubuti .

Kwa mujibu wa shirika hilo ingawa katika miongo miwili iliyopita kiwango cha ukataji miti kimepungua lakini hakiko sawia katika kanda zote kwani katika baadhi ya kanda hususani Afrika na Amerika ya Kusini kiwango cha ukataji miti kiko juu na ni cha kutisha.

Peter Csoka afisa misitu wa FAO, amesema lengo kuu la mkutano huo ni kutoka kwenye mtazamo kwenda kwenye hatua hasa kwa kutathimini vichocheo vya sasa vya ukataji miti, kubaini fursa zilizopo za kuchagiza upandaji miti, kufufua maeneo ya hifadhi ya misitu na kutoa mapendekezo kuhusu hatua za kisera zitakazochukuliwa na nchi  na jumuiya ya kimataifa kuhakikisha misitu inalindwa kwa ajili ya mustakbali wa dunia na maendeleo endelevu.

Csoka amesema na wanachotaraji kwenye mkutano huo utakaomalizika kesho

(SAUTI YA PETER CSOKA)

“Tunatumai kwamba mkutano huu utachangia kwa kiasi kikubwa kutambua haja ya kushirikiana miongoni mwa sekta na pia tunatarajia ujumbe, mawazo na dhana na mapendekezo yatapewa kipaumbe katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa misitu utakaofanyika Mei kwa ajili ya kutathiminiwa na uwezekano wa utekelerzaji wake.”

Audio Credit
Selina Jerobon
Audio Duration
1'58"
Photo Credit
Picha: FAO