Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lugha ya mama ni muaroabaini wa kufanikisha SDGs- UNESCO

Lugha ya mama ni muaroabaini wa kufanikisha SDGs- UNESCO

Pakua

Kila wiki mbili zinapopita, lugha moja ya asili inayotumika duniani inatoweka! Amesema Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoaj wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni, UNESCO, Audrey Azoulay katika ujumbe wake wa siku ya lugha ya mama duniani hii leo.

Hawa ni wamasai katika moja ya burudani zao kupitia lugha yao ya mama! UNESCO inasema  kuwa lugha ya mama ni msingi wa kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, SDGs, kwani matumizi ya lugha ya mama yanawezesha mtu kupokea maarifa mapya kwa urahisi kuliko kupitia lugha ya mapokeo au lugha ya kigeni.

 Ili kufahamu uhusiano huo, nimezungumza na Dkt. Elifuraha Laltaika kutoka Tanzania ambaye ni mtaalamu huru wa jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu watu wa asili nikamuuliza ni kwa vipi?

 (Sauti ya Dkt. Elifuraha Laltaika)

 UNESCO inasema kuwa lugha ni zaidi ya mawasiliano, hili nalo linathibitika vipi Dkt. Laltaika?

 (Sauti ya Dkt. Elifuraha Laltaika)

 Mahojiano kamili na Dkt. Laltaika ambaye pia ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira nchini Tanzania yatapatikana kwenye wavuti wetu www.news.un.org/sw

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
1'39"
Photo Credit
Elifuraha Laltaika.(Picha:Idhaa ya Kiswahili/ Joseph Msami)