Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanamazingira Afrika mashariki wanolewa Bujumbura

Wanamazingira Afrika mashariki wanolewa Bujumbura

Pakua

Katika jitihada za kuchagiza ajenda ya maendeleo endelevu ya mwaka waka 2030, Umoja wa Mataifa na washirika wake wameendeleza kampeni mbalimbali duniani kuhimiza serikali na asasi za kiraia kuelemisha jamii katika utunzaji wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi.

Katika ukanda wa nchi zilizoko mashariki mwa Afrika kama Tazanzia, Kenya, Uganda, Rwanda, na Burundi serikali zimekutana katika kuelimisha jamii zao kuwekeza katika uhifadhi wa misitu, bahari, mito na mbuga za wanyama kama sehemu ya kampeni za kulinda mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani Kibuga ameudhuria mkutano huo ambapo wadau kutoka asasi za kirai za Afrika Mashariki wamejumuika ili kupata mafuzo ya kuthibiti athari za mabadiliko ya tabianchi jijini Bujumbura, Burundi. Nini kimejiri katika mafunzo hao ? ungana naye katika makala hii

Audio Credit
Ramadhani Kibuga
Audio Duration
4'10"
Photo Credit
Mtaalamu wa misitu akipima kipenyo cha mti kama sehemu ya kuhifadhi miti na misitu. (Picha:FAO)