Skip to main content

Wanawake wa mashinani ni waleta mabadiliko

Wanawake wa mashinani ni waleta mabadiliko

Pakua

Ukitaka kupanga miji vizuri, husisha wanawake! Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na makazi, UN-Habitat, Maimunah Mohd Sharif  wakati akifungua mkutano wa tisa wa jukwaa la miji,WUF9 ulioanza leo huko Kuala Lumpur Malaysia.

Amesema ni muhimu kushirikisha wanawake katika upangaji miji ili kufanikisha lengo namba 11 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu miji jumuishi akigusia nukuu aliyowahi kuelezwa kuwa..

(Sauti ya Maimunah Mohd Sharif)

“Iwapo unataka kupanga mji vizuri, uliwa wanawake. Hii ni kwasababu tunatumia miji kila siku, na miji haijapangwa na kusimamiwa kwa misingi ya kijinsia. Wanawake ni wadau wakuu wa miji lakini bado wana sauti finyu kwenye uendeshaji.”

Naye mwakilishi wa wanawake wa mashinani kutoka Kenya Violet Kibute amezungumzia jinsi wanawake wa mashinani ambao ndio wa kwanza kuamka na wa mwisho kulala walivyotambua changamoto zao na kuungana hadi hivi sasa wanashiriki kwenye vikao vya serikali vya kutatua shida zao.

(Sauti ya Violet)

“Awali walionekana ni wanufaika na walengwa, lakini baada ya kuanza kujumuika na kujadiliana na serikali ,jukumu lao linabadilika na kuwa waleta mabadiliko. Na hivi ndivo madaraka kwenye jamii yanabadilika kwani wanawake wanaitwa kwenye vikao vya serikali ili kupitisha tu mipango ambayo serikali imeanza. Lakini baadaye sasa wanawake ndio wanakaribisha  serikali isikilize matatizo  yao na kupendekeza hatua za kuboresha na ndipo sasa mtazamo wa serikali kwa wanawake unabadilika.”

Maudhui ya mkutano huo ni miji kwa wote mwaka 2030- utekelezaji wa ajenda mpya ya miji.

Audio Credit
Siraj Kalyango
Audio Duration
2'5"
Photo Credit
Mafunzo kwa wanawake ni sehemu ya kuwajengea uwezo ili waweze kushiriki kikamilifu katika masuala ya uongozi. (Picha: Julius Mwelu/ UN-Habitat)