Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN-Tanzania imefanya mengi kutuelimisha kuhusu SDGs- Rahma

UN-Tanzania imefanya mengi kutuelimisha kuhusu SDGs- Rahma

Pakua

Wiki hii katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani limefanyika kongamano la kimataifa la vijana la mwaka 2018, lenye lengo la kuwajumuisha vijana katika malengo ya maendeleo endelevu au SDGs.

Tulipata fursa ya  kukutana na mmoja wa washiriki wa jukwaa hilo Rahma Abdallah Mwita ambaye ni kijana kutoka Tanzania. Rahma ni mmoja wa wanzilishi wa mtandao  wa vijana kuhusu mabadiliko ya tabianchi ( Youth Climate Change Activist Network).

Katika  sehemu ya kwanza ya mahojiano na Patrick Newman wa Idhaa ya Kiswahili,  Rahma amezungumzia nafasi ya vijana wa kitanzania katika masuala ya Tabianchi, maendeleo, ajira na usawa kijinsia katika jamii ya kitanzania,  ikiwa ni utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Audio Credit
Patrick Newman akizungumza na Rahma Abdallah Mwita
Audio Duration
5'22"
Photo Credit
UN News/Patrick Newman