Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN kuimarisha utawala wa sheria Haiti- MINUJUSTH

UN kuimarisha utawala wa sheria Haiti- MINUJUSTH

Pakua
Ujumbe mpya wa  Umoja wa Mataifa nchini Haiti MINUJUSTH,umeanzisha  mbinu mpya ya kuimarisha utawala wa sheria na kuunga mkono vikosi vya usalama  nchini humo.Mbinu  hizo ni pamoja na utekelezaji wa  ulinzi shirikishi baina ya  vyombo vya usalama, asasi za kiraia, vyiongozi wa kisiasa na wananchi ambapo amani usalama, haki  na utawala wa sheria vinapatiwa  kipaumbele.Akizungumzia kwa undani mpango huo, Susan Page ambaye ni mkuu wa ujumbe huo mdogo wa Umoja wa Mataifa baada ya ule wa zamani, MINUSTAH kumaliza kazi yake amesema,..(Sauti ya Susan Page)“Jambo la kipekee kuhusu MINUJUSTH ni kwamba ujumbe huu unajikita zaidi katika masuala ya utawala wa sheria, na wajibu wetu hapa ni kushirikiana na serikali ya Haiti katika kutoa mwongozo na mafunzo kwa vikosi vya usalama ili kuimarisha usalama, utawala wa sheria na haki za kibinadamu “ Na ili kufahamu MINUJUSTH imejipanga vipi kuhakikisha utawala wa sheria Haiti unasimamiwa vipi, Bi. Page amesema(Sauti ya Susan Page)“Ofisi yetu ipo Port Au Prince, pia tuna timu yetu ambayo hufanya safari za kwenda na kurudi katika mikoa mbalimbali kwa ushirikiano na vyombo vya wananchi katika jitihada za kutafuta kujua mahitaji yao kisheria ,haki za binadamu na pia maendeleo endelevu hususan katika swala namba 16 la amani, haki na utawala wa kisheria.”MINUJUSTH ilianza rasmi kazi zake Oktoba mwaka jana ikichukua nafasi ya MINUSTAH, ikiwa na lengo la kushirikiana na serikali ya Haiti katika kuimarisha ulinzi na pia kujenga misingi ya kulinda haki za binadamu.
Photo Credit
endera la Umoja wa Mataifa lainuliwa katika sherehe ya ufunguzi wa Ujumbe mpya wa Umoja wa Mataifa kwa Usaidizi wa Haki nchini Haiti (MINUJUSTH). Picha: Logan Abassi / MINUJUSTH