Masharti ya kipekee yanusuru familia maskini Ufilipino

3 Januari 2018

Changamoto za nchi nyingi zinazoendelea zinatokana na baadhi ya viongozi kukosa dira. Hata hivyo mwelekeo unaweza kubadilika iwapo viongozi watagutuka na kuwekeza  katika elimu hususani kwa vijana.

Benki ya dunia na washirika wake wamekuwa mstari wa mbele katika jitihada za kuwekeza katika elimu kupitia mipango mbalimbali kwa kuzingatia mifumo ya nchi husika.
Mathalani nchini Ufilipino mbinu iliyotumiwa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na serikali imeleta nidhamu katika siyo tu matumizi ya familia bali pia ushiriki wa familia kwenye afya na elimu na mtoto na zaidi ya yote vijana kupata elimu ya juu. Je nini kinafanyika?  Ungana na Patrick Newman katika makala hii.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud