Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wanolewa huko DRC

Wanawake wanolewa huko DRC

Pakua
Harakati za kujumuisha wanawake katika usuluhishi na utatuzi wa migogoro huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia yaCongo, DRC zinashika kasi baada ya wanawake kushiriki kwenye warsha ya kuwapatia stadi hizo. Ikiandaliwana mkutano wa kimataifa wa Maziwa Makuu, ICGLR, warsha hiyo imefanyika katika zama za sasa zilizogubikwa na mvutano wa kisiasa kutokana na vuta ni kuvute kuhusu uchaguzi mkuu nchini humo na baadhi ya watu wakitaka Rais Joseph Kabila ajiuzulu kuelekea uchaguzi. Mwakilishi kutoka ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO Taib Diallo amesema wanawake wamepatiwa stadi za kushiriki kwenye utatuzi wa migogoro, halikadhalika mamlaka husika zinapatiwa ushawishi wa kusongesha amani nchini humo. Azimio husika namba 2348, la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilikuwa moja ya nyaraka zilizotumikaambapo pamoja na mambo mengine linataka wanawake kushiriki katika ngazi zote za uchaguzi pamoja na masuala ya amani na usalama. Zaidi  ya wanawake 60 kutoka mashirika mbalimbali ya kiraia walishiriki pamoja na watetezi wa haki za wanawake na wataalamu aw masuala ya usongeshaji amani, mazungumzo, maridhiano na stahmala.
Photo Credit
Warsha kuhusus ujumuishwaji wa wanawake katika usuluhishi na utatuzi wa migogoro huko nchini DRC. Picha: MONUSCO