Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghasia DRC 5 wauawa; Guterres alaani

Ghasia DRC 5 wauawa; Guterres alaani

Pakua

Ghasia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. DRC zimesababisha vifo vya watu 5 na wengine zaidi ya 120 wamejeruhiwa.

Ghasia hizo zinafuatia mtafaruku uliozuka kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama katika mji mkuu wa kinshasa na miji mingine mbambali mbali nchini DRC.

Yaelezwa kuwa Waandamanaji wanataka Rais Joseph Kabila ajiuzulu wakati huu upigaji kura ukisubiriwa mwisho wa mwaka.

 Kufuatia hali hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia msemaje wake ameeza kuwa anaendelea kufuatilia kwa ukaribu hali hiuo ya kisiasa nchini DRC kufuatia maandamano hayo ya hivi karibuni.

Katibu Mkuu ametoa wito kwa pande zote kinzani  kuendelea na mikakati ya kutafuta suluhu katika migogoro inayoendelea na pia kufikia makubaliano kuhusu tarehe ya uchaguzi ili kupata viongozi watakaosimamia mchakato wa amani nchini DRC.

Photo Credit
Katibu mkuu Antonio Guterres