Saratani yasababisha hasara ya dola bilioni 46
Ripoti mpya kutoka katika kituo cha kimafaida cha utafiti wa ugonjwa wa saratani duniani,IARC inasema ugonjwa huo imezigharimu nchi zenye uchumi wa kati ,kiasi cha dola za kimarekani bilioni 46 tangu mwaka 2012.
Katika ripoti hiyo Dkt Alisona Pearce kutoka IARC amesema nchi hizo zijulikanazo kama BRICS, ambazo ni China, Brazil, India, Afrika ya kusini na Urusi ambazo zina idadi ya asilimia 40 ya watu duniani, zinatumia gharama kubwa katika utafiti na pia matibabu ya ugonjwa wa saratani, hivyo kuathiri nguvu kazi na kusababisha hasara kubwa katika ukuaji wa uchumi.
Kati ya nchi hizo China peke yake imetumia dola bilioni 28 katika kukabiliana na saratani ya ini, maambukizi ya virusi vya homa ya ini aina ya B na magonjwa mengine ,Urusi wao ni saratani ya ini na shingo, wakati Brazil, Afrika kusini na India wanakabiliwa na saratani ya ini, mdomo na shingo itokanayo ya matumizi yaliokithiri ya tumbaku.
Mkurugenzi wa IARC Dkt Christopher Wild katika utafiti wa shirika hilo amesema ili kujuia hasara hiyo kubwa katika ukuwaji wa uchumi lazima nchi za BRICS ziweke katika sera za kitaifazitakazo zingatia udhibiti wa matumizi ya tumbaku, mipango ya chanjo ya awali na pia uchunguzi wa mapema wa saratani.