Skip to main content

Hema linalohimili mabadiliko ya tabia nchi ni nuru kwa wakimbizi Uganda

Hema linalohimili mabadiliko ya tabia nchi ni nuru kwa wakimbizi Uganda

Pakua

Wakimbizi wa Sudani Kusini waishio kwenye makazi ya wakimbizi ya Maaji -Adjuman kaskazini mwa Uganda sasa wananeemeka na huduma ya afya kupitia hema maalumu linalohimili mabadiliko ya tabia nchi. Hema hilo la aina yake duniani limetolewa kama zawadi kwa wakimbizi hao na wanafunzi wa chuo kikuu cha Makerere baada ya hema hilo kuwawezesha kushinda tuzo ya ubunifu wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Kwa maelezo zaidi tuungane na Siraj kalyango

Photo Credit
Hema maalumu linalohimili mabadiliko ya tabia nchi, Uganda. Picha: James Makumbi